Kutoka na ubora mkubwa wa Liverpool ndani ya uwanja unawafanya kupiga pesa za maana hata kuwa klabu inayowalipa mastaa wake vizuri duniani.
Nguvu hiyo ya kipesa imewasaidia kuwaweka karibu na kwa muda mastaa wao kama Mohammed Salah,Sedio Mane na Roberto Firmino ambao wote walipiga madili yenye dau nono mwaka jana.
Liverpool inataka kumpa pia dili hilo beki wao kisiki Virgil Van Dijik kwa kumuongezea mshahara mkubwa pamoja na wachezaji wengine muhimu ili waendelee kubaki Merseyside kwa mda mrefu.
Ofisa mkuu wa uendeshaji kwenye klabu ya Liverpool,Andy Hughes alisema kuwa uwekezaji huo sio wa kitoto hasa kwenye soka linalowahusisha klabu zinazotumia pesa kwa wingi kama Real Madrid ,Barcelona na Manchester United.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Liverpool kwa sasa wanashika namba tatu kwenye ligi kuu England kwa timu zinazogawa mishahara mikubwa baada ya sasa wakipata kumpa dili jipya Van Dijik litakalomfanya awe beki anayelipwa pesa nyingi Duniani.