Home Makala Miezi Miwili Yamkuta Beki Wa Valencia

Miezi Miwili Yamkuta Beki Wa Valencia

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu  ya Valencia, Alessandro Florenzi ametengwa kwa miezi miwili sasa baada ya kukutwa na maambukizi ya aina tofauti ikiwemo virusi vya Corona.

Awali Florenzi alitengwa peke yake kwa mwezi mmoja baada ya kuugua tetekuwanga(Chikenpox) lakini sasa ametengwa kwa mwezi mmoja baada ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mchezaji huyo alijiunga na Valencia kwa mkopo Januari mwaka huu akitokea katika klabu ya Roma na amefanikiwa kucheza dakika 160 msimu huu kabla ya La Liga kusimamishwa kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

banner

Beki huyo alikosa mechi dhidi ya Atletico Madrid, Atalanata na Real Sociedad, lakini baadaye alicheza dhidi ya Real Betis na alikaa benchi mechi dhidi ya Alaves na Atalanta.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited