Mshambuliaji anayekipiga ndani ya klabu ya Orlando Pirates,Justine Shonga bado yupo kwenye vichwa vya mabosi wa Simba wanaotaka kuipata saini yake huku kinachowapasua kichwa ni dau lililowekwa mezani.
Â
Mabosi wa Simba wana hamu kubwa ya kumpata nyota huyo licha ya pesa inayohitajika kuanzia shilingi milioni 800, pia upo uwezekano wa kupungua na kumnyakua mwamba huyo ndio maana mazungumzo yanaendelea.