Nyota anayekipiga ndani ya Sao Paulo ,Dani Alves amesema kuwa haitakuwa vibaya kama atastaafia ndani ya klabu ya Boca Junior.
Alves ambaye ni beki aliyekipiga pia Barcelona amesema kuwa alikuwa anaipenda timu hiyo kwa muda mrefu kabla ya kutumika ndani ya Barca na Sao Paulo.
“Unajua ninaipenda nimekuwa nikiipenda kwa muda mrefu klabu ya Boca sio kwa sababu watu wanaiongelea hapana ni klabu kubwa nimegundua ina kitu cha tofauti,” alisema Alves.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.