Home Makala Fernandes Asambaza Chakula Kwa Waathirika Wa Corona

Fernandes Asambaza Chakula Kwa Waathirika Wa Corona

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa kati katika klabu ya Manchester United ,Bruno Fernandes alijiunga na wahisani wengine katika kupambana na virusi vya Corona kwa kusambaza msaada wa chakula Ureno.

Fernandes mwenye umri wa miaka 25 alirudi nyumbani nchini Ureno baada ya ligi ya Premia kusitishwa mwezi Machi kutokana na janga la Corona.

Kutokana na unyenyekevu wake alijiunga na wengine katikaa kusambaza vyakula wananchi wa Ureno baada ya kuombwa kufanya hivyo na kiongozi wa kikundi cha mashabiki Fernando Madureira.

banner

“Bruno aliuliza jinsi ya kujiunga na kundi hilo na baadae akawa tayari kusaidia hata alienda kusambaza vyakula hivyo kwa waathirika wa Corona akiwa na Madureira”alisema Cassama ambaye ni nyota wa Real Ibra alipokuwa akimsifia nyota huyo.

Fernandes kwa sasa amerejea Uingereza kwa maandalizi ya ligi ya premia inayotarajia kuanza wiki chache zijazo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited