Cristian Pulisic mwenye miaka 21 anayekipiga kwenye klabu ya Chelsea akitokea ndani ya Borussia Dortmund amesema kuwa siku ya kwanza wachezaji wenzake walimchunia ndani ya gari walipokuwa njiani kuelekea mazoezini.
Nyota huyo aliyesajiliwa majira ya joto aliongeza kuwa hakuna aliyetaka kumfahamu, kumsemesha wala kumtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya jambo lililomfanya ajiulize mara mbili yupo sehemu gani.
“Siku tatu za mwanzo hakuna mchezaji aliyekuwa akinijali kila mtu aliniona ni mtu wa kawaida ila nilipoanza kufunga na kutoa pasi za mabao wakaanza kunipa ushirikiano,” alisema Pulisic
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.