Home Soka Simba sc Waingia Kambini Rasmi

Simba sc Waingia Kambini Rasmi

by Dennis Msotwa
0 comments

Wachezaji na benchi la ufundi la klabu ya Simba sc leo wameingia rasmi kambini kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara ambayo inatarajiwa kurejea hivi karibuni kufuatia kusimamishwa na serikali ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kipa wa Klabu ya Simba Beno Kakolanya akiwa sambamba na beki wa Klabu hiyo Kennedy Juma wakiwasili Kambini leo asubuhi.

Klabu hiyo imeingia kambini katika hoteli ya Sea Escape ambapo huweka kambi kwa muda mrefu kujiandaa na ligi hiyo.

Simba inatarajiwa kuendeleza wimbi lake la ushindi huku ikiongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi zaidi ya kumi huku Azam fc na Yanga wakimfuatia.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited