Taarifa kutoka nchini Hispania zinaeleza kuwa staa wa klabu ya Barcelona Lionell Messi na kocha wa klabu hiyo Quique Setien wamemaliza tofauti zao baada ya kufanya mazungumzo ili kuinusuru klabu hiyo katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
Messi amekua akimkosoa kocha huyo pamoja na baadhi ya mastaa klabuni hapo hasa kutokana na mbinu mbovu za kocha na kutojitoa kwa mastaa hao hali iliyopelekea kukosa ubingwa wa Laliga ambao umeenda kwa Real Madrid licha ya Barca kuongoza ligi kwa kipindi kirefu.
Matunda ya mazunguzo hayo yameonekana baada ya kuifunga Alaves mabao 5 siku ya Jumapili na sasa wanajiandaa kuwavaa Napoli ili kuhakikisha klabu hiyo haimalizi msimu bila kombe.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.