Baada ya nahodha wa yanga Papy Tshishimbi kusuasua kusaini mkataba mpya,mambo yamemgeukia kwani Yanga ni kama wamemfungia vioo baada ya kuamua kusajili wachezaji wengine katika nafasi yake.
Zilianza kama tetesi lakini sasa kuna uhakika mkubwa kiungo mkabaji kutoka As Vita ,Mukoko Tunombe anaweza kutua kuchukua nafasi yake.
Lakini pia za chinichini ni kuwa Yanga imetua pale Kagera Sugar ikihitaji saini za viungo wawili walioibeba timu hiyo msimu uliomalizika ambao ni Zawadi Mauya na Awesu Awesu.
Mauya ni kiungo mkabaji pia ni mtu wa kazi kwelikweli hivyo kama Yanga watafanikiwa kumnasa ni wazi Tshishimbi hatakuwa na nafasi kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria.
Ikumbukwe kwamba Eng:Said alishamalizana kila kitu na Tshishimbi na akapewa mkataba ili asaini na kuurudisha ila hali imekuwa tofauti akihitaji pesa zaidi.
Tshishimbi atajilaumu mwenyewe kwani alipewa mkataba tangu mwezi March lakini akasuasua kuusaini ikielezwa anataka pesa zaidi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga inayosukwa sasa sio ya kubembeleza wachezaji ,inaelezwa wachezaji wanapewa ofa kulingana na mchango na kiwango chao katika msimu uliomalizika.
Kwa wale ambao watagomea ofa hizo wataruhusiwa kuondoka ili nafasi zao wasajiliwe wachezaji bora zaidi yao.
Cc:Yangasportsupdates