Home Makala Ni PSG Vs Bayern Munich Jumapili

Ni PSG Vs Bayern Munich Jumapili

by Dennis Msotwa
0 comments

Bayern Munich imeitungua mabao 3-0 Lyon kwenye mchezo wa nusu fainali hatua ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya jana.

Bao la kwanza na la pili lilipachikwa na Gnabry dakika ya 18 na 33 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huku lile la tatu lilifungwa na mshambuliaji Lewandowski dakika ya 88.

Fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya inatarajiwa kuchezwa Agosti 23 siku ya Jumapili kati ya PSG dhidi ya Bayern Munich ambapo wote wamepata matokeo yanayofanana kwenye nusu fainali.

banner

PSG ilitinga hatua ya fainali kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Leipzig hivyo bingwa ataonekana Jumapili atakayesepa na taji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited