ALAIN Thiery kutoka nchini Cameroon amejifunga kwa miaka miwili ndani ya Azam FC yenye makazi yake Chamazi leo Agosti 24.
Mshambuliaji huyo amesaini dili hilo akiwa kama mchezaji huru aliyemaliza kandarasi yake ndani ya Fortuna Du Mfuo ya Cameroon.
Mabosi hao wa Azam wamefunga kwa mchezaji huyu baada ya wengine kuwatambulisha jana kwenye siku yao(Azam Festival)iliyofanyika katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na msanii wa kizazi kipya wa bongo fleva,Alikiba na wasingeli akiwa Msagasumu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.