Klabu ya Yanga Sc imejinasia saini ya Said Ntibazonkiza kutokea timu ya taifa Burundi akiwa kama mchezaji huru baada ya kukosa timu kwa muda mrefu.
Ntibazonkiza amesaini dili la miaka miaka miwili Yanga ambayo kwa sasa ipo chini ya kaimu kocha mkuu, Juma Mwambusi.
Nyota huyo ambaye pia alipata dili ndani ya Vital ‘O’ msimu wa 2019 lakini hakupata nafasi kucheza kikosi cha kwanza ,alikuwa ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kwenye mchezo wa jana ambapo walivaana na Taifa Stars na kuwapa kichapo cha bao 1-0.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.