Washambuliaji wawili wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza pamoja na Yacouba Sogne waliokua na majeraha waliyoyapata katika michuano ya mapinduzi Cuo visiwani Zanzibar Bado kidogo tu warudi katika hali yao ya kawaida baada ya kupona majeraha.
Awali wachezaji hao walikua wakisumbuliwa na majeraha mbalimbali lakini kwa mujibu wa kocha Cedrick Kaze tayari wachezaji hao wameanza mazoezi kurejea katika utimamu kamili wa mwili.
Wachezaji hao wamekua na mchango mkubwa kwa timu hiyo hasa katika mechi za ligi kuu nchini hivyo kurejea kwa ni faraja kwa klabu hiyo iliyoanza rasmi mazoezi kujiandaa na awamu ya pili ya ligi kuu nchini inayotarajiwa kuanza Februari 13.