Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho la Azam Sports Confederation Cup baada ya jana kuifunga African Lyon mabao 3-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Mabao ya Ibrahim Ajib dakika za 10 na 44 pamoja na bao la dakika za mwishoni la Perfect Chikwende lilitosha kuipeleka timu hiyo katika hatua inayofuatia ya michuano hiyo ambapo watakutana na Kagera Sugar ambao walifanikiwa kuwafunga Eagle Stars kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Nassoro Kapama na Yusuph Mlipili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.