Home Soka Man Utd yavutwa shati na Newcastle

Man Utd yavutwa shati na Newcastle

by Dennis Msotwa
0 comments

Ligi kuu soka nchini England imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa mchezo mmoja tu uliozikutananisha Newcastle united dhidi ya Manchester united kwenye dimba la St James Park.

Weneyji waliuanza mchezo huo kwa kasi sana kwa kufanya mashambulizi hatari na ya kushtukiza na hatimaye kupata bao la mapema dakika ya 7 tu ya mchezo kupitia nyota wa kikosi hicho Saint Maximin akimalizia vizuri kazi yake mwenyewe baada ya kuwachambua vizuri mabeki wa Man Utd wakiongozwa na Harry Maguire.

Mpaka mechi inakwenda mapumziko Newcastle walikua mbele kwa 1-0,kipindi kilianza kwa kocha wa Utd Ralf kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Fred na Greenwood kisha kuwaingiza Cavan na Sancho ambao kidogo walianza kuwasumbua wenyeji,dakika ya 71 Cavan aliisawazishia timu yake kwa kumalizia vizuri pasi ya beki wa kulia Diogo Dalot.

banner

Baada ya hapo mechi ilikuwa ni ya kushambuliana kwa zamu lakini ni Newcastle ndio waliokuwa hatari zaidi kwa mashambulizi yao,shukrani kwa De Gea ambaye aliokoa mchomo hatari wa Almiron vinginevyo Newcastle wangeondoka na alama zote tatu.

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mechi kadhaa ambapo Crystal Palace watacheza dhidi ya Norwich,Southampton dhidi ya Tottenham,Watford dhidi ya West Ham,Leicester dhidi ya Liverpool huku mchezo baina ya Arsenal na Wolves ukiahirishwa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited