Home Soka Chelsea yang’ang’aniwa,City mwendo mdundo epl

Chelsea yang’ang’aniwa,City mwendo mdundo epl

by Dennis Msotwa
0 comments

Ligi kuu soka nchini Uingereza imeendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa mechi mbili ambazo Chelsea walikuwa wakicheza dhidi ya Brighton huku Manchester city wakicheza na Brentoford.

Chelsea walikuwa nyumbani darajani walishindwa kupunguza gepu la pointi kati yake na Man city kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na kugawana alama.Romelu Lukaku aliwapa uongozi ‘The Blues’ dakika 40 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona.

Brighton walirudi kwa kasi kipindi cha pili kwa kutawala mchezo kwa asilimia kubwa huku wakifanya mashambulizi mengi ya hatari ambayo hata hivyo hayakufanikiwa kutinga wavuni kutokana na uimara wa mlinda mlango Benjamin Mendy aliyekuwa kwenye ubora.Hata hivyo Danny Welbeck aliisawazishia Brighton dakika ya 90+1.

banner

Vinara wa ligi hiyo Manchester city wao wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachapa nyuki wa London Brentford kwa goli 1-0 na kumaliza mwaka wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ya Malkia.

 

Ligi hiyo itaendelea tena usiku wa leo kwa mechi moja ambapo mashetani wekundu Manchester united watakuwa nyumbani Old Trafford kuwakaribisha wabishi Burnley.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited