Home Soka HARRY KANE FITI KUIVAA LIVERPOOL

HARRY KANE FITI KUIVAA LIVERPOOL

by Sports Leo
0 comments


Harry Kane, anatarajiwa kukwea pipa na kikosi chake cha Tottenham siku ya Jumatano kuifuata Liverpool kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mshambuliaji huyo amekuwa kwenye maandalizi ya kikosi kinachojiandaa kuivaa Liverpool kwenye fainali itakayopigwa siku ya Jumamosi alikuwa nje kutokana na kusumbuliw na majeruhi. Meendeleo ya mshambuliaji huyo yamekuwa yakiridhisha hali inayotoa nafasi kubwa kwake kuweza kuanza kwenye kikosi kitakachoshuka uwanja wa Wanda Metropolitano. Meneja wa Totthenham, Mauricio Pochettino anahitaji kumpa nafasi mshambuliaji huyo ili kujua kiasi gani amekuwa imara baada ya kupata majeruhi. "Kumuanzisha yeye ndani ya kikosi ndiyo kitu ambacho ninakifikiria itakuwa ni maamuzi yangu mwenyewe kumuazisha ama kutomuanzisha kwenye mchezo huo ama michezo mingine, itategemea na namna atakayofanya kama tukishinda itakuwa furaha tukipoteza ni mbaya kwetu," amesema.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited