Home Soka Cameroon yafuzu 16 bora AFCON 2021

Cameroon yafuzu 16 bora AFCON 2021

by Dennis Msotwa
0 comments

Wenyeji wa michuano ya kombe la Mataifa Afrika Cameroon wamekuwa wa kwanza kutinga hatua ya mtoano wa michuano hiyo baada ya hapo jana kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Wahabeshi Ethiopia na kufikisha pointi sita kileleni mwa kundi A.

Ethiopia walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 4 kupitia kwa Hotessa Dawa kabla ya Cameroon kuchomoa bao hilo dakika nne baadae kupitia kwa mshambuliaji wa Lyon ya Ufaransa Karl Toko Ekambi na kupelekea mchezo huo kwenda mapumzika kwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili wenyeji waliutawala zaidi mchezo kwa kushambulia lango la Ethiopia kwa kiasi kikubwa na hatimaye dakika ya 53 nahodha Aboubacar kuandika bao la pili.Dakika ya 55 Aboubacar aliifungia Cameroon bao la tatu na kuifanya akaunti yake ya mabao katika michuano hiyo na kufikia manne.

banner

Karl Toko Ekambi alifunga bao la nne na bao lake la pili kwenye mchezo huo na kuwafanya wapate ushindi mnono na kufuzu hatua inayofuata.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Burkina Faso walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Cape Verde na kufufua matumaini ya kusonga mbele wakisubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Ethiopia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited