Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Iman Kajula amefafanua kuhusu madai ya klabu hiyo kudaiwa posho na wachezaji wa klabu hiyo hali iliyosababisha kupoteza mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Azam Fc.
Simba sc ilipoteza kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara huku taarifa zikisambaa kwa kuna mgomo baridi miongoni mwa wachezaji kutokana na madai yao ya posho za michezo mbalimbali.
Madai hayo yalithibitishwa na Ahmed Ally meneja wa habari wa klabu hiyo lakini imemlazimu bosi huyo kujitokeza na kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo.
“Timu yetu imeshatoa Bonus zaidi ya Billion 1.1 na kiasi kilichobaki ni milioni 20 pekee tena ni Bonus ya Ligi ya ndani, wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Billion 1.1 inashindwaje kulipa milioni 20 haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia Kajula aliendelea kusema kuwa “Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi.””- Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.
Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa Bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapandane zaidi kwenye kile wanachokipambania.