Mshambuliaji William Edgar Ajiunga na Dodoma Jiji Fc kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Singida Black Stars iliyokua inammiliki kwa makubaliano ya pande mbili na sasa rasmi ni mchezaji wa Dodoma Jiji Fc.
Mshambuliaji huyo alikuwa kwa mkopo Fountain Gate Fc akitokea Singida Black Stars ambapo msimu huu ulioisha ameutumia katika klabu hiyo na kufanikiwa kuonyesha kiwango bora kilichowavutia mabosi wa Dodoma jiji kumsajili huku pia ujio wa kocha mpya Annicet Kiyazadi ukisisitiza kukamilika kwa dili hilo.
Dodoma Jiji Fc kumsajili mshambuliaji huyo imelamba dume kutokana na kuwa na uwezo wa kutumika kama winga zote za kulia na kushoto ama kucheza kama kiungo mshambuliaji akitumia zaidi nguvu na kasi yake katika kusukuma mashambulizi kwa wapinzani.
Dodoma Jiji inajipanga kwa ajili ya msimu ujao ambapo tayari imeachana na kocha Mecky Mexime pamoja na wasaidizi wake na imempa mkataba kocha wa zamani wa Tabora United Annicet Kiyazadi ambaye anatua klabuni hapo kuiongoza kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na kombe la shirikisho la Crdb.
Â