Home Makala Fifa Yaamuru Rayon Kumlipa Robertinho Mamilioni

Fifa Yaamuru Rayon Kumlipa Robertinho Mamilioni

by Dennis Msotwa
0 comments

Shirikisho la soka Duniani (Fifa), limeiamuru klabu ya Rayon Sports Fc ya nchini Rwanda kumlipa kocha wake wa zamani Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ Dola za Kimarekani Elfu 22.5 [zaidi ya Milioni 30 za Rwanda] kwa kumfukuza kinyume na sheria wakati alipokua akiifundisha klabu hiyo msimu uliopita.

Kocha Robertinho ambaye alisimamishwa kazi na Rayon Sports kwa sababu ya ugonjwa, aliwasilisha malalamiko ya kutaka kulipwa mshahara wake kuanzia Januari 2025 hadi mwisho wa msimu Juni 2025 ambao alisitishiwa kinyume na makubaliano ya kimkataba baina yake na timu hiyo.

Katika barua kwa pande zote mbili ya Agosti 12, 2025, FIFA inasema Rayon Sports wana siku 45 pekee kulipa $22,500 na endapo wakishindwa kulipa kiasi hicho basi wanaweza kukumbana na adhabu kali zaidi ikiwemo kufungiwa kusajili wachezani wa ndani na nje ya nchi mpaka pale watakapolipa malipo hayo.

banner

Fifa Yaamuru Rayon Kumlipa mamilioni Robartinho-sportsleo.co.uk

Pia endapo klabu hiyo haitatekeleza inaweza kufungiwa kusajili wachezaji wa ndani na nje misimu mitatu na adhabu hiyo inaweza pia kuongezeka kadri inavyoendelea kukaidi maagizo hayo wa wasimamizi wakuu wa soka duniani.

Robertinho, ambaye alikuwa akilipwa Dola 5,000 kwa mwezi, hajalipwa kwa miezi sita wakati alipokua ameondoka klabuni hapo kwa sababu ya maradhi yaliyokua yakimsumbua ambapo ilimlazimu arejeee nyumbani kwa Brazil kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi wa afya yake mpaka pale alipopona kabisa.

Mbrazil huyo ambaye aliwahi kuifundisha klabu ya Simba sc amepata kibarua kipya hivi karibuni, ambapo ataifundisha Jeddah SC ya Saudi Arabia kwa msimu ujao wa 2025/26.

Robertinho ni moja ya makocha wenye majina makubwa barani Afrika hasa Afrika mashariki ambapo alipata kuvifundisha vilabu vya Vipers Fc ya nchini Uganda ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa baada ya kukisuka kikosi hicho na kukifanya kuwa maarufu Afrika mashariki ambapo kilikua hakifungiki kirahisi hali iliyompa ulaji katika klabu ya Simba sc ambao walivunja mkataba wake na kutua nchini Tanzania.

Hata hivyo kocha aliondoka nchini kwa fedheha kubwa akiruhusu kikosi chake kufungwa mabao 5-1 na Yanga sc Novemba 5 2023 hali iliyosababisha kocha huyo kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Abdelhack Benchika ambaye naye hakudumu kikosini humo na kuja kocha Fadlu Davids ambaye yupo na timu hiyo mpaka sasa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited