Home Makala Ajibu,Boko Kuikosa Ud Songo

Ajibu,Boko Kuikosa Ud Songo

by Sports Leo
0 comments

Rasmi imethibitishwa nyota wawili wa klabu ya Simba sc Ibrahimu Ajibu na John Boko wataukosa mchezo wa kalbu bingwa Afrika dhidi ya Ud songo y Msumbiji baada ya wawili hao kuwa majeruhi.

Ajibu alikosekana katika mchezo wa kwanza nchini msumbuji kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata akiwa katika kambi ya timu ya taifa hivyo anakosa utimamu wa mwili baada ya kuanza mazoezi hivi karibuni.

“ Kwa sasa ninaendelea vizuri na nimeanza mazoezi hivi karibuni lakini sipo fiti kwa mchezo ujao na Ud Songo hivyo najipanga kuwa fiti zaidi ili kuona naisaidia timu yangu kwenye michezo ijayo” alisema staa huyo alijiunga na Simba akitokea Yanga akiwa ameisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili baada ya kufunga mabao sita na kutoa assisti 17.

banner

Kwa upande wa Boko alipata majeraha katika mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Azam fc hali iliyomlazimu kumpisha Cletous Chama na hivyo kwa mujibu wa kocha wa kalbu hiyo Patrick Aussems ataukosa mchezo huo baada ya ripoti ya madaktari kuonyesha atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited