Klabu ya soka ya Al Hilal ya Sudan imependekeza jina la kocha wa Simba Sc raia wa Afrika kusini Fadru Davis kuwa kipaumbele Chao Cha kwanza kukinoa kikosi chao kuanzia msimu ujao.
Mabosi wa klabu hiyo wamefikia uamuzi huo baada ya kuwa na uhakika kuwa kocha wao wa sasa Florent Ibenge anatimka kikosini humo mwishoni mwa msimu huu kutokana na kuwa na ofa nono.
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ni kuwa Uongozi wa Al Hilal Fc unaona kabisa Fadlu ndiye kocha mwenye CV kubwa na uwezo wanaoutaka na watakua tayal kuvunja mkataba alionao pale Simba Sc wa mwaka mmoja aliobakisha ili tu wamnase kikosini humo.
Fadlu Davis inafikiria mbadala wa kocha wao Florent Ibenge Raia wa Dr Congo ambaye anaondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kutamatika mwezi huu huku wakiwa tayari na orodha ya makocha wengine ambao kama mbadala wa Fadlu.
Hata hivyo mabosi hao hawana uhakika wa asilimia mia kumnasa Fadlu kutokana na msimamo wako ambapo tayari amekataa ofa za klabu kadhaa akiona kama bado hajamaliza kazi yake katika kikosi hicho kutokana na kuwa na projekti maalumu msimbazi.