Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) Emmanuel Amunike amelishitaki shirikisho la soka nchini (Tff) kwa shirikisho la soka duniani (Fifa) kutokana na kutolipwa stahiki zake.
Kocha huyo raia wa Nigeria anayeishi nchini Hispania alitimuliwa na Tff baada ya kuiongoza Taifa stars kufanya vibaya katika michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon ) yaliyofanyika nchini Misri.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Completesports.com na Punching.com inaonesha kocha huyo amefikisha malalamiko yake Fifa ili kuweza kupata utatuzi baada ya kusubiri malipo hayo kwa muda mrefu toka mwezi julai.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.