Juhudi za wachezaji wa Arsenal uwanjani siku ya jana umewasaidia mbele ya mabingwa wa ligi kuu England,Liverpool baada ya kuwafunga mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani Emirates.
Mabao ya Arsenal yalipachikwa na Alexandre Lacazette dakika ya 32 na Reiss Nelson dakika ya 44 huku bao lililofungua mchezo kwa upande wa Liverpool lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 20.
Kocha mkuu Arsenal,Mikel Arteta amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kupata ushindi mbele ya mabingwa kwani wana timu imara ya ushindani ambayo imewapa ubingwa ila vijana wake walikuwa na juhudi mchezoni jambo lililowapa matokeo mazuri.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Kucheza na mabingwa na kupata matokeo ni jambo jema hii inatupa picha ya kujua kule ambako tunakwenda kama si kwa wakati huu basi itakuwa kwa ajili ya wakati ujao” alisema Arteta