Ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Emirates klabu ya Arsenal imeshindwa kuvuna alama katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa vijana wa kocha Jurgen Klopp wa Liverpool.
Ikianza mchezo kwa kasi Arsenal ilionekana kama inakwenda kushinda mchezo huo huku kinda Martin Ondegard akionekana kutakata eneo la kiungo lakini mipango ya kikubwa ya Liverpool ilizima ndoto hiyo japo mpaka mapumziko matokeo yalikua bila bila.
ilimchukua dakika kadhaa kipindi cha pili Diogo Jota ambapo dakika ya 54 alijaza kimiani bap la uongozi na bao la pili lilijazwa kimiani na Robert Firmino dakika ya 62 japo staa huyo aliingia akitokea benchi katika mchezo huo uliotazamwa na mashabiki elfu 59 waliokuwepo jukwaani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ushindi huo unawasukuma Liverpool kupunguza gepu la alama mpaka kufikisha 69 dhidi ya 70 za Manchester City walioko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza huku ikiwa imesalia michezo michache ligi imalizike.