Kiungo Khalid Aucho ambaye alikua na majeruhi kwa wiki kadhaa tayari amerejea kikosini Yanga sc ambapo ameonekana akifanya mazoezi na wenzake baada ya kumaliza programu ya utimamu wa mwili.
Kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga sc aliumia katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar jeraha ambalo lilipona lakini alijitonesha katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Uganda alikoitwa wiki chache zilizopita katika michezo ya kimataifa.
Aucho anakuja kuongeza ubora wa safu ya kiungo ya Yanga sc ambayo ilipwaya kutokana na kuumia kwake pamoja na kiungo Feisal Salum hivyo kufanya kikosi kuwa na viungo wa asili wa eneo la kati wawili pekee ambao ni Zawadi Mauya na Salum Abubakari ‘Sure Boy’.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha Nabi sasa atakua anafurahia kurejea kwa Aucho kutokana na michezo migumu iliyo mbele yake dhidi ya Namungo Fc na Simba sc ambayo itapisha wiki pekee huku michezo hiyo ikibeba picha halisi ya safari ya ubingwa ya klabu hiyo ambao iliukosa kwa takribani miaka minne mfululizo.