Azam Fc imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Octoba 12,uwanja wa Azam Complex.
Bao la kwanza kwa Azam lilipachikwa na Mudathir Yahya dakika ya 24 huku anayekitamani kiatu cha dhahabu VPL,Prince Dube alipachika mabao mawili dakika ya 43 na 44.
Kader wa Azam Fc alipachika bao la nne lenye ushindi dakika ya 49 na kuipa ushindi timu yake katika uwanja wao wa nyumbani uliopo Chamazi wa Azam Complex.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezo huo ulikuwa wa maandalizi kwa tiimu zote mbili kwani Azam Fc inajiandaa na mchuano wa raundi ya sita wa ligi kuu bara huku Fountain Gate ukijiandaa na ligi daraja la kwanza.