Katika maandalizi kuelekea mechi dhidi ya Simba sc katika mchezo wa ngao ya hisani Azam imeifunga Namungo mabao 8-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa chamazi complex hapo jana.
Azam ambao pia wanakabiliwa na mechi ya marudiano dhidi ya Fasil Kanema katika kombe la shirikisho itawavaa wanamsimbazi ambao waliwafunga goli tatu katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita huku Meddie Kagere akifunga mabao mawili katika mechi hiyo.
Mabao ya Azam dhidi ya timu hiyo iliyopanda daraja yalifungwa na Djodi,Seleman,Sure Boy,Kangwa,Chilunda,Chirwa,Kassim na Idd Kipagwile alihitimisha karamu hiyo ya mabao kwa penati.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.