Klabu ya Azam Fc Yamsajili Kitambala ambapo kiungo mshambuliaji wa AS Maniema amekamilisha usajili kwa kusaini mkataba wa miaka miwili klabuni hapo mapema wiki hii.
Nyota huyo wiki hii alikua Tanzania na tayari amerejea kwa ajili ya makubaliano ya mwisho na kisha kusaini mkataba huo na kurejea nyumbani Congo baada ya kumalizana vyema na matajiri wa Chamazi na anajiandaa kwa maandalizi ya msimu mpya.
Mshambuliaji huyo ni pendekezo la kocha mpya wa klabu hiyo Frolent Ibenge ambaye nae amesaini mkataba wa kuifundisha timu na sasa ameingia mstari wa mbele katika zoezi la usajili wa mastaa kikosini humo.
Shitambala ni Mshambuliaji anayenyumbulika akiweza kucheza nafasi zote za juu za ushambuliaji huku pia akicheza kama kiungo mshambuliaji pale inapohitajika.
Mshambuliaji huyo anatajwa kuwa ni hatari akiwa na nguvu za kutoka kupambana na mabeki wa timu pinzani huku akiwa na uzoefu wa kuitumikia timu ya Taifa ya Congo DRC sambamba na vilabu vikongwe nchini humo kama AS Vita na Tp Mazembe.
Azam Fc imemsajili mshambuliaji huyo kuchukua nafasi ya mshambuliaji Allasane Diarra ambaye ametemwa klabuni hapo kutokana na kuwa na kiwango kisichoridhisha huku akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.