Mchezo wa kirafiki baina ya Azam Fc na Tp Mazembe umemalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 za mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Ndola nchini Zambia.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ambao Azam Fc walialikwa na Tp Mazembe ulikua wa kasi na kosa kosa nyingi huku ukiwa na ufundi wa hali ya juu ambapo Azam Fc iliandika bao la kwanza na pekee katika mchezo huo dakika ya 36 likifungwa na Kipre Junior baada ya mpira kushinda kipa wa Mazembe.
Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika 20 pekee ambapo dakika ya 57 Zemanga Soze aliisawazishia Tp Mazembe kwa shuti kali baada ya mpira kuzagaa nje ya eneo la 18 la Azam Fc.
Azam Fc imepata kipimo sahihi kuelekea raundi ya pili ya michuano ya kimataifa ambapo ilipata bahata ya kuanzia katika raundi hiyo huku Simba na Yanga sc pamoja na Geita Gold Fc zilianzia raundi ya awali ya michuano ya kimataifa.