Home Makala Bakuli Lagoma Gormahia

Bakuli Lagoma Gormahia

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Gormahia inayoshiriki ligi kuu nchini Kenya imeshindwa kukusanya kiasi cha kutosha kwenye harambee maalumu ya kuichangia timu hiyo ili ipate fedha za kuwezesha kucheza mchezo wa hatua ya mtoano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya USM Algers.

Harambee hiyo ambayo ilifanyika siku ya jumanne wiki hii ilijikuta ikihudhuriwa na watu wachache tofauti na matarajio huku wageni muhimu kama mlezi wa timu hiyo Raila Odinga akishindwa kufika kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Wengine ambao hawakufika licha ya kupata mwaliko huo ni Gavana Mike sonko na mbunge George Aladwa ambao piahaikufahamika sababu ya kushindwa kufika kwao.

banner

Fedha ambazo zimekusanywa kwa mujibu wa mwenyekiti wa timu hiyo Ambrose Rachier hazitoshi kugharamia mechi hiyo ambayo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

“Hatujafanikiwa kukusanya kiasi cha kutosha kugharamia malazi na hoteli,Hatukukusanya fedha nyingi kwa sababu asilimia kubwa ya wageni hawakufika”.

Timu hiyo awali ilikuwa inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa na sasa inakabiliwa na wakati mgumu baada ya kampuni hiyo kujitoa kutokana na kuongezeka kwa kodi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited