Mario Balotelli ameamua kumtema nyota wa Juventus na Ureno Christiano Ronaldo katka kikosi chake cha wakati wote.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amewaorodhesha wachezaji wawili tu wa ligi kuu na amemchagua gwiji wa Brazil Ronaldo kuongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Lionel Messi.
Thierry Henry alimtaka Balotelli kutaja kikosi cha wachezaji 11 cha mwisho katika ‘Puma Football Instagram’ ,mshambuliaji huyo alimchagua mchezaji mwenzake wa zamani ,Yaya Toure na nyota wa Liverpool Steven Gerrad kucheza nafasi ya katikati katika timu ya Brencia.
Balotelli alishinda taji la ligi kuu akiwa na Manchester City mwaka 2012 kabla hajaondoka katika klabu hiyo mwaka 2o13 na kujiunga na Milan .
Nyota huyo alirejea England akiwa Liverpool mwaka 2014 lakini alishindwa kufikia malengo akiwa katika klabu hiyo yenye maskani yake Anfield.