Winga Peter Banda amekubali kuondoka katika klabu ya Simba sc baada ya kupata ofa sehemu nyingine na kumaliza mgogoro wake na klabu hiyo ambayo ilikua na nia ya kumtoa kwa mkopo.
Inasemekana kuwa Banda aligomea kutolewa kwa mkopo akitaka aachwe moja kwa moja akatafute malisho sehemu nyingine lakini kuwasili kwa ofa hiyo kumelifanya jambo hilo kuwa rahisi kwa pande zote mbili.
Kuondoka kwa Banda kutarahisisha usajili wa Luis ambapo Simba sc inapambana kukamilisha dili la winga huyo pamoja na kipa mpya huku tayari kikosi ilikuwa na nyota 12 wa kigeni kwa mujibu wa sheria ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lakini kuibuka kwa ofa ya Banda imewapa nguvu Simba sc kumalizana na Al Ahly ili kumrejesha Luis huku pia ikidaiwa kuwa Sakho nae tayari amepata timu hivyo anaweza kuondoka.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Usajili wa kipa na Luis unasubiriwa kwa hamu na wanasimba wengi huku wakiwa na mioyo safi kuwaruhusu Banda na Sakho kuondoka kutokana na orodha ya majembe waliyosajili.