Kiungo maestro wa klabu ya Yanga sc Yannick Bangala yupo hatihati kuwavaa Dodoma jiji katika mchezo wa ligi kuu nchini utakofanyika jioni ya tarehe 15/5/22 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na kocha mkuu wa klabu hiyo Nasreddine Mohamed Nabi ni kuwa kiungo huyo amefiwa na kaka yake hivyo kumpanga inategemea na hali yake itakavyokua baada ya kufanya nae kikao cha mwisho kama anaweza kucheza.
Bangala amekua ni kiungo muhimu katika klabu ya Yanga sc akicheza vizuri eneo la kiungo pamoja na beki wa kati kwa ufasaha huku akiwa na utulivu mkubwa katika kuanzisha mashambulizi ya timu hiyo hivyo kumkosa inaweza kuwa na pengo kwa klabu hasa katika michezo ya mwishoni yenye presha kubwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.