Home Makala Barbara Aula Caf

Barbara Aula Caf

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka Afrika Magharibi zinadai kuwa Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Simba sc Barbara Gonzalez ameteuliwa kuwa makamu wa Rais wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya vilabu ya Caf pamoja na usimamizi wa mfumo wa leseni kwa klabu.

Katika uteuzi huo mpya ambao utadumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2022-2024 Barbara atamsaidia Rais wa kamati hiyo ambaye ni Ahmed Yahya huku kukiwa na watu wengine hasa kutoka Afrika Magharibi katika mataifa makubwa na yenye maendeleo makubwa kisoka.

Barbara tangu ateuliwe kuwa Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc akichukua nafasi ya Mohamed Dewji amekua karibu sana na wadau wa soka Afrika hasa Shirikisho la soka hilo kiasi amepata koneksheni za kutosha kuweza kuisaidia klabu ya Simba sc katika mambo mbalimbali kimataifa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited