Timu ya Yanga sc ipo njiani kwenda mkoani Kilimanjaro kuweka kambi ya muda kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana utakaofanyika mjini Gaborone nchini humo.
Yanga imelazimika kuweka kambi mkoani humo ili kuzoea mazingira ya baridi la Gaborone ambayo hayatofautiani na hali ya hewa ya mkoani humo ambapo pia timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Polisi ya mkoani humo na Fc Leopard ya nchini Kenya ili kujiweka fiti kwa ajili ya mechi hiyo.
Katika msafara huo wachezaji waliokua nje ya kikosi Kelvin Yondani na Juma Abdul wameungana na wenzao kuweka kambi mkoani humo.
Yanga itakua na kazi ya kuhakikisha inapata ushindi au sare ya magoli kuanzia mawili ili iweze kufuzu hatua inayofuata baada ya kutoka sare ya bao moja moja katika mechi ya awali iliyofanyika nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.