Home Makala Bayern Yazidi Kujikusanyia Mataji

Bayern Yazidi Kujikusanyia Mataji

by Sports Leo
0 comments

Bayern Munich ya Ujerumani imefanikiwa kutwaa ubingwa wa German Super Cup dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali ulichezwa jana bila uwepo wa mashabiki viwanjani kutokana na kudhidi kujikinga na virusi vya Corona.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa umemalizika baada ya Bayern Munich kuwatungua Dortmund mabao 3-2 ambapo bao la kwanza kwa Munich lilipachikwa dakika ya 18 na Corentin Tolisso huku Thomas Muller akiona nyavu dakika ya 32 na dakika ya 82 Joshua Kimmich alipachika bao la tatu la ushindi.

Dortmund walipata mabao mawili kupitia Julian Brandt dakika ya 39 na Erling Braut Halaand dakika ya 55.

banner

Ushindi huo unamfanya Thomas Muller aandike rekodi ya kuwa mchezaji wa kijerumani mwenye mafanikio zaidi baada ya kutwaa taji lake la 27.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited