Home Makala Berkane Wakutana na Rungu Caf

Berkane Wakutana na Rungu Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Rs Berkane ya nchini Morroco imepigwa faini ya jumla ya dola za kimarekani laki moja na elfu nane kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya klabu ya Simba sc uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika kosa la kwanza klabu ya Berkane imepigwa faini ya dola elfu nane kutokana na mashabiki wa klabu hiyo kuwarushia chupa za maji wachezaji wa klabu ya Simba sc huku Majid Madrane ambaye ni Ofisa wa klabu hiyo akifungiwa kwa miezi 12 kutojihusisha na soka kutokana na utovu wa nidhamu ambapo aliingia uwanjani na kushinikiza wachezaji wa klabu hiyo kugomea mchezo ambao ulisimama kwa takribani dakika 5.

Kutokana na kosa hil0 klabu ya Rs Berkane imepigwa faini ya dola laki moja na kufanya faini ya jumla kufikia kiasi cha dola laki moja na elfu nane huku baada ya mechi hiyo ya Dar es Salaam, RS Berkane waliwasilisha barua ya kulalamika kuonewa jijini Dar es Salaam na malalamiko makubwa yalikuwa kwa mwamuzi Jaques Ndala wa Congo, ambaye anaendelea kutimiza majukumu yake.

banner

Rs Berkane inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Asec Mimosa kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited