Home Makala Berkane Yanogewa na Mukwala

Berkane Yanogewa na Mukwala

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco inavutiwa na huduma ya mshambuliaji Steven Mukwala (25) kutoka Simba sc ambapo sasa mabosi wa klabu wamewasilisha ofa rasmi klabuni hapo.

Taarifa zinadai kuwa  Berkane imeweka mezani ofa ya USD 300,000 (Tshs 790M) kwa Simba Sc ili kupata saini ya Steven Mukwala ambaye ni raia wa Uganda kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo mabosi wa Simba Sc wamepata kigugumizi kutoa jibu la moja kwa moja kutokana na kiwango cha Mukwala kupanda ghafla na sasa amekua mshambuliaji tegemeo klabuni hapo.

banner

Mukwala alikosa nafasi mbele ya Lionel Ateba lakini kutokana na juhudi zake sasa amekua mshambuliaji tegemeo klabuni hapo akifunga mabao muhimu katika ligi kuu na michuano ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika ligi kuu mpaka sasa mshambuliaji huyo ana mabao 12 mpaka huku akiwa na uhakika wa kufunga zaidi katika michezo mitatu iliyobakia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited