Bado haijafahamika kama mshambuliaji wa Simba sc John Boko atakua fiti kucheza mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ud Songo baada ya kupata maumivu katika mchezo dhidi ya Azam Fc.
Boko aliumia kipindi cha kwanza na nafasi yake ilichukuliwa na Cletous Chama na mpaka sasa bado anaendelea na matibabu kupitia jopo la tiba la klabu hiyo.
Licha ya kumkosa Boko Simba inatarajiwa kuwa na Kipa Aishi Manula ambaye alikosa mchezo wa kwanza baada ya kupata majeraha akiwa na timu ya taifa.