Home Makala Bruno Aondoka Singida Fg

Bruno Aondoka Singida Fg

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji Bruno Gomez ameamua kuvunja mkataba na klabu yake ya Singida Fountain Gate Fc kutokana na klabu hiyo kushindwa kutimiza baadhi ya vipengele vya kimkataba baina yao hivyo kumlazimu staa huyo raia wa Brazil kuamua kufungasha virago vyake.

Gomez alijiunga na Singida Fg mwaka 2022 ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili na baada ya kuutumikia kwa mafanikio aliongeza tena mkataba mwanzoni mwa msimu huu ambao ameamua kuuvunja rasmi kutokana na baadhi ya vipengele vya kimkataba kukiukwa na klabu hiyo.

banner

Katika barua yake kwa mashabiki staa huyo alisema kwamba sababu ya kuondoka klabuni hapo ni uvunjaji wa mkataba kwa upande wa klabu hivyo uamuzi huo umekua bora kwa pande zote ambazo zinahusika.

Bruno alihitajika na Simba sc mwishoni mwa msimu uliopita lakini klabu hiyo iligoma kumuuza lakini msimu huu wakati wa dirisha dogo iliwatoa kwa mkopo mastaa kama Joash Onyango,Duke Abuya,Marouf Tchakei na wengine kwenda Ihefu Fc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited