Shirikisho la Soka barani Afrika (caf) limeufungulia uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika katika michezo ya hatua ya robo fainali na nusu fainali ya michuano iliyochini ya Shirikisho hilo baada ya kujiridhisha na ubora wake.
Awali Caf waliufungia uwanja huo kutokana na kushuka ubora wa sehemu ya kuchezea ambapo baada ya maboresho kadhaa Caf ilituma timu ya ukaguzi machi 20 ambao walijiridhisha na ubora wa uwanja huo na sasa wameamua kuufungulia.
Kutokana na Caf kuufungulia uwanja huo sasa uhakika mechi ya Simba Sc dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kuchezwa April 9 2025 itafanyika katika uwanja huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc sasa ipo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa hatua ya kwanza siku ya April 2 2025 ambapo kisha watarejea nchini kumalizia mchezo wa pili.
Kufunguliwa kwa uwanja huo sasa kunawapa nafuu Simba sc kutokana na kuwa na rekodi nzuri wanapocheza katika uwanja huo.