Home Makala Carlinhos Awashukuru Mashabiki Yanga

Carlinhos Awashukuru Mashabiki Yanga

by Sports Leo
0 comments

Nyota mpya wa mabingwa wa kihistoria Tanzania bara, Yanga Sc “Carlos Stenio Guimaraes do Carmo” maarufu kama Carlinhos ametoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wote wa klabu hiyo kwa mapokezi makubwa ambayo yatabaki historia kwake.

Carlinhos aliwasili jana uwanja wa Mwl Julius Kambarage Nyerere saa saba mchana ambapo alikutana na umati mkubwa wa mashabiki wa Yanga tayari kumpokea na kumkaribisha nyumbani Jangwani.

Mashabiki hao walikuwa ni wengi sana kana kwamba waliikonga nafsi za nyota huyo na kujiona amefikia sehemu salama na kwa watu wenye ukarimu wa dhati kwani umoja wao ulishindwa kuzuilika hadi serikali ikaamua kuingilia ili kutuliza fujo zilizotokana na furaha.

banner

Carlinhos ambaye ni raia wa Angola amesema kuwa amefarijika sana kujiunga na Yanga Sc ambayo ni timu kubwa na tayari ameuona ukubwa wake kabla hajaingia uwanjani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited