Cedrik Kaze ambaye ni kocha mpya wa Yanga ameanza na safu ya ushambuliaji katika program zake za mazoezi kuhakikisha anapunguza ukame wa mabao katika kikosi chake.
Akianza na Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ akimtaja kuwa anashindwa kuwapa pasi washambuliaji wenzake ambao ni Michael Sarpong,Yacouba Songne, Waziri Junior na Tuisila Kisinda.
Safu hiyo ya ushambuliaji wa Yanga mpaka sasa imefanikiwa kufunga mabao saba pekee ikiruhusu bao moja baada ya kucheza michezo mitano tangu kuanza kwa ligi kuu bara.
Kaze alisema kuwa anaamini uwezo wa washambuliaji wake aliowakuta ingawa wanashindwa kuonesha umahili wao katika kufunga mabao kutokana na viungo wa timu hiyo kama Carlinhos kukosa mbinu za pamoja kuwapigia pasi za mwisho za kufunga mabao.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Nimeanza kuiboresha safu ya ushambuliaji ili kuhakikisha natengeza muunganiko mzuri wa viungo na washambuliaji ambao kabla ya kuja kwangu haukuwepo “alisema Kaze