Home Makala Chama Kuikosa Singida FG

Chama Kuikosa Singida FG

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Cletous Chama ataukosa mchezo wa ufunguzi wa michuano mifupi ya ngao ya jamii dhidi ya Singida Fountain Gate kutokana na kufungiwa michezo mitatu iliyochini ya shirikisho la soka nchini TFF.

Chama alifungiwa kutokana na kuwa na adhabu hiyo aliyopewa baada ya kutenda tendo lisilokua la kiungwana baada ya kumkanyanga mchezaji AbalKassim Seleman wa Ruvu Shooting katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu nchini ambao Simba sc waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Adhabu hiyo ya michezo mitatu itamfanya staa huyo kukosa mchezo huo pekee kutokana na kwamba alishaitumikia msimu uliopita alipokosa michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union hivyo ataungana na kikosi katika mchezo wa ama fainali ama mshindi wa tatu katika michuano hiyo mifupi itakoyohusisha timu nne za Simba sc,Azam Fc,Yanga sc na Singida Fountain Gate Fc.

banner

Hata hivyo kukosekana kwa Chama hakutajwi kuwa kama ni pengo kubwa kwa klabu hiyo kutokana na aina ya wachezaji wapya iliowasajili ambapo kwa sasa mastaa kama Saido Ntibanzokiza,Aubin Kramo,Leandre Onana wanaweza kuziba pengo hilo bila wasiwasi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited