Beki wa klabu ya Simba Sc Che Malone Akalia Kuti Kavu Simba Sc kutokana na kuwa katika hatihati ya kusalia klabuni hapo kutokana na viongozi wa klabu hiyo kutoridhishwa na uwezo wake huku ikidaiwa kuwa kocha Fadlu Davis anahitaji beki mwingine kikosini humo.
Hata hivyo pia beki huyo upo hatua za mwisho za mazungumzo ya kujiunga na USM ALGER (USMA) ya Algeria kwenda kukipiga nchini humo baada ya mabosi wa klabu hiyo kuridhishwa na uwezo wa beki huyo.
Hadi sasa ni asilimia 90 Che Malone anaondoka ndani ya Simba Sports Club Kutokana na ofa hiyo ya Waalgeria kuwa nzito kiasi cha kuvutiwa nayo ikiwemo mshahara na fedha ya kusainia mkataba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mbali na ofa hiyo,Che Malone Fondoh pia ana ofa ya MAS (Maghreb Fez) ya ligi kuu ya Morocco ila USM ALGER (USMA) ndio ambao wapo kwenye hatua nzuri za kumalizana na Che Malone hadi sasa.