Kocha wa klabu ya Yanga sc Nasredine Nabi amethibitisha kuwa winga Chico Ushindi anasumbuliwa na maralia hivyo ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold Fc.
Chico aliyesajiliwa dirisha dogo la usajili mwezo januari akitokea Tp Mazembe mpaka sasa bado hajaonyesha makeke kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara klabuni hapo.
Toka asajili amecheza michezo ya kirafiki dhidi ya Mbuni Fc na ule wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Polisi Tanznia ambapo aliingia dakika za mwishoni.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezaji huyo kwa mujibu wa Nabi yuko hatihati kucheza mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na maralia yeye na Djuma Shabani.