Yanga Sc imepata ushindi leo Octoba,3,2020 wa mabao 3-0 mbele ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu bara uliofanyika uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga Sc, Carlos Carlinhos alianza kuzivamia nyavu za Coastal dakika ya 48 mara baada ya kutoka mapumziko ya kipindi cha kwanza na hapo aliandika bao la kwanza kwa klabu hiyo.
Bao la pili lilipachikwa na Haruna Niyonzima dakika ya 53 huku dakika ya 63 Yocouba Sogne alizikonga mioyo za mashabiki wao kwa kumalizia bao la tatu ambao ni la ushindi mkubwa na kuweza kunyakua alama tatu mbele ya Coastal Union.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Coastal Union baada ya kufungwa walizidi kucheza kama kipindi cha kwanza wakizdi kutengeneza mashambulizi ambayo hayakuzaa matunda yoyote mbele ya wanajangwani hao.