Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limetangaza kuwa ule mchezo wa ngao ya jamii baina ya vilabu vya Simba Sc dhidi ya Yanga sc(K/koo Derby) sasa utafanyika septemba 16 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo mchezo huo ndio utafungua rasmi pazia la ligi kuu nchini.
Kwa mujibu wa TFF tayari klabu hizo mbili zimepewa taarifa rasmi ili kuanza maandalizi kuelekea mchezo huo ambao lazima mshindi apatikane uwanjani hapo kwa maana kutakua na kombe huku fedha zinazopatikana kupitia viingilio na matangazo moja kwa moja hupelekwa kusaidia jamii.
Yanga sc imechukua kombe hilo msimu uliopita ambapo ilimfunga Azam Fc kwa mabao 4-1 katika fainali iliyofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo msimu huo michuano hiyo ilifanyika kama ligi iliyoshirikisha timu nne za Simba sc,Yanga sc,Singida Black Stars na Azam Fc.
Msimu huu TFF imeamua kubadili tena utaratibu ambapo michuano hiyo itajumuisha timu mbili pekee ambapo kwa mujibu wa kanuni ilipaswa iwe bingwa wa ligi kuu dhidi ya bingwa wa kombe la shirikisho ambapo kanuni hiyo inaelekeza kuwa endapo bingwa wa ligi kuu akawa pia ndio bingwa wa kombe la shirikisho basi michuano hiyo itahusisha mshindi wa kwanza na wa pili wa ligi kuu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali baina ya timu hizo ambazo zote msimu huu zimesajili mastaa wa kutosha kuziba mapengo ya wazi tangu zikutane katika mchezo wa mwisho wa msimu wa ligi kuu ambao Yanga Sc ilishinda kwa mabao 2-0 na kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini.
Simba Sc chini ya kocha Fadlu Davis ambaye amepewa jukumu la kufanya usajili wa mastaa msimu na tayari amefanikiwa kuwanasa mastaa mbalimbali wa ndani na nje ya nchini kama vile llasane Keita,Rushine De Reuck,Anthony Mligo,Neo Maema,Jonathan Sowah,Mohamed Bajaber,Morice Abraham,Charles Semfuko huku pia wakijiandaa kutangaza mchezaji mwingine wa mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa ambapo taarifa zinadai wanapambana kukamilisha usajili wa Wilson Nangu na Yakub Selemani ambnao tayari dili hizo zipo mwishoni tayari kukamilika.
Kwa upande wa Yanga sc yenyewe imewasajili mastaa Offen Chikola,Lassine Kouma,Mousa Balla Conte,Andy Boyeli,Celestine Acua,Abubakar Nizar Othman,Mohamed Hussein,Mohamed Doumbia,Abdulnasir Mohamed Casemiro pamoja na Edmund John.